usuli
Hospitali ya Amana ilianzishwa mnamo mwaka 1954 kama Zahanati, mnamo 1982 iliboreshwa kuwa kituo cha afya. Miaka minane baadaye iliboreshwa tena kuwa Hospitali ya Manispaa / Wilaya na ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali kama Hospitali ya Rufaa ya Mkoa mnamo Oktoba, 2010. Hospitali hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Manispaa ya Ilala hadi Julai, 2018 ambapo ilihamishwa rasmi na kuwa chini ya wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana iko kando ya barabara ya Uhuru katika Kata ya Ilala - Manispaa ya Ilala - Jiji la Dar es salaam, idadi ya wakazi wake inakadiriwa kuwa 1,220,611 kulingana na sensa ya Kitaifa ya Mwaka 2012.
Hospitali inahudumia/inaona wagonjwa wa nje (OPD) 800-1200 kwa siku kati ya hao wagonjwa …….. hadi ……… hulazwa kwa siku, Hospitali ina idadi ya vitanda 341.
Aidha, hospitali inapokea wagonjwa ….kutoka vituo… vya binafsi na vya Serikali kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Halmashauri za Manispaa zinazopakana nayo;(Temeke,Ubungo,Kigamboni na Kinondoni).
Kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za ziada (uchunguzi na huduma zaidi) hupelekwa hospitali ya Muhimbili (MNH) au Mloganzila.